Sunday, August 17, 2008

Hakika tutashinda daima

Yapaswa kusimama imara kupigania haki yetu wote kwa pamoja hapo ndio tutakomboa haki yetu tuliyodhulumiwa tangi baba wetu wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere afariki dunia, waliobaki wanatutesa kama sisi hatuna haki na rasilimali zetu, lakini saa yao imekaribia kwani ukombozi wetu umefika, ila yatupasa kusimama dhabiti kupambana na mafisiazuni.

Watanzania wenzagu sasa simameni kupigania haki yenu tusikate tamaa kwani haki yetu ni ya kwetu sisi sote, kwanini tuwaachie hawa waendelee kutudhurumu? kwani Mungu aliwapa wao peke yao? Hii ni mali yetu yatupasa tupiganie hata kwa kupoteza damu zetu.

Wednesday, August 13, 2008

Nguvu ya Fikra

Nguvu ya Fikra ni haki ya msingi ambayo binadamu anatakiwa kuwa nayo, kwani maisha ya binadamu yametawaliwa na fikra, binadamu akifikri jambo baya hakika atatenda jambo hilo, na akifikri jambo zuri vilevile atatenda jambo hilo, kwahiyo ukifikri vibaya matokeo yake ni mabaya na ukifikri mazuri matokeo yake ni mazuri kwani binadamu anatenda jambo ambalo analifikria.

Kwahiyo binadamu yatupasa kujikomboa kifikra ili kupata uhuru wetu wa kufikri, wengi wa binadamu tunatawaliwa kifikra na watu wengine ambapo ni jambo baya sana kutawaliwa kifikra hasa ikiwa anayekutawala akiwa ni viongozi wako au mtu ambaye unamtegemea kwa kila kitu kwani hapa ndio atakufanya uwe mtumwa wa fikra zake.

Mapinduzi ya fikra yanahitajika sana katika maisha ya bianadamu ili kufuata misingi ya maisha bora yasiyokuwa na unyonyaji, udhurumiaji wa haki za misingi, saa ya ukombozi imefika tusikubali kunyanyasa kifikra na viongozi wetu kwani tukikubali hilo watatutumia ili kutudhulumu haki yetu pasina kuwagundua.

Wewe Mfanyakazi, Mkulima, simama uitetee haki yako, pigania ukombozi wako wa fikra daima kwani huu ndio uhuru wako wa kujikomboa kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni, kisaikolojia hii ni mfumo wako wa kujikomboa na uongozi wa wanyonyaji, wahujumu mali za umma, wanaojari masirahi yao, na wasio na chembe hata moja ya huruma bali ukiwaona ni binadamu kumbe roho zao ni Simba mla watu.

"Tanzania Daima Mapinduzi ya Fikra ni Uhuru wetu"